Uchumi wa taifa la Tanzania ulipanuka kwa asilimia 5.2 mwaka
2018 kulingana na benki ya dunia iliosema katika katika ripoti yake kuu mwaka
huu ambapo imetofautiana na takwimu zilizotolewa na serikali hiyo za kuimarika
kwa uchumi huo.
Kulingana na chombo cha habari cha Reuters, waziri wa fedha
nchini Tanzania alikuwa ameliambia bunge mwezi uliopita kwamba ukuwaji huo
ulikuwa wa asilimia 7 mwaka uliopita.
Katika ripoti hiyo, kulingana na Reuters, benki kuu ya dunia
ambayo hufanya hesabu zake kwa kutumia data ilizonazo pia ilikadriria kwamba
uchumi huo utakua kwa asilimia 5.4 ikiwa ni chini ya asilimia 7.1 inayokadiriwa
na serikali.
Kwa nini Nato inasema makombora ya Urusi ni hatari?
Atembea kilomita 10,000 kushabikia Afcon
Ni kwanini talaka zinaongezeka?
Ukuaji wa mwaka uliopita uliathiriwa na kushuka kwa viwango
vya uwezekazji, mauzo katika mataifa ya kigeni na ukopeshaji katika sekta ya
kibinfasi, ripoti hiyo imesema.
Kulinga na Reuters, data inayohusiana na matumizi, uwekezaji
na biashara inonyesha kwamba ukuaji huo ulipungua mwaka 2018, imesema ripoti
hiyo.
Rais John Pombe Magufuli alianzisha mpango wa kuimarisha
sekta ya viwanda baada ya kuchukua hatamu mwaka 2015, akiwekeza mabilioni ya
dola katika miundo msingi, ikiwemo barabara ya reli, kufufua uchukuzi wa
kitaifa wa angani pamoja na kiwanda cha umeme.
Lakini hatua ya serikali kuingilia sekta ya uchimbaji wa
madini pamoja na ile ya kilimo imesababisha kupungua kwa uwekezaji katika sekta
hizo katika taifa hilo linalotajwa kuwa la tatu kwa ukubwa kiuchumi Afrika
mashariki, ilisema ripoti hiyo iliochapishwa na Ruters.
Tanzania yataka ripoti iliyovuja ya IMF kupuuzwa
Kulingana na chombo hicho cha habari uwekezaji wa kigeni wa
moja kwa moja umepungua maradufu tangu 2013, huku ukuaji wa mikopo katika sekta
ya kibinafsi ukipungua na kufikia chini ya silimia 4 mwaka 2018, ikiwa ni
kiwango cha chini cha wastani kati ya 2013-16.
Ripoti hiyo ya benki ya dunia inajiri kufuatia ripoti ambayo
haikuchapishwa ya hazina ya shirika la fedha duniani IMF mnamo mwezi Aprili
ambayo pia ilihoji jinsi rais Magufuli anavyoendesha uchumi wa taifa hilo.
Kulingana na reuters ripoti iliovuja ambayo ilionekana na
chombo hicho cha habari, iliishutumu serikali kwa kukandamiza uchumi huo
kupitia sera ''zisizotabirika mbali na zile zinazoingilia kati'', ikisema kuwa
ukuwaji wa katikati wa uchumi huo utakua kati ya asilimia 4-5 kwa mara nyengine
ikiwa ni chini ya makadirio ya serikali.
Katika ripoti yake, benki ya dunia WB imesema kuwa ukuaji wa
kiwango cha uwekezaji ulishuka kwa sababu ya serikali kushindwa kuafikia
malengo yake ya matumizi katika miradi ya maendeleo.
Ripoti hiyo inasema kwamba uchumi huo unaweza kunawiri kwa
asilimia 6 kufikia 2021 iwapo kutakuwa na uimarikaji wa wa sekta ya biashara,
uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja mbali na uwekezaji mwengine wa kibinafsi,
ilisema benki hiyo.
Tanzania yakanusha kuzuia ripoti ya IMF
Viashiria vingine vya kiuchumi pia vimeonyesha kupungua kwa
kasi ya ukuaji wa uchumi.
Upungufu huo uliongezeka hadi asilimia 5.2 ya pato la taifa
katika mwaka uliokwisha Januari 2019, kutoka asilimia 3.2 mapema mwaka mmoja
uliopita.
Reuters inasema kwamba thamani ya mauzo ya nje imepungua
karibu 4% mwaka jana, kwa sababu serikali imepiga marufuku mauzo ya nje ya
korosho bidhaa inayoingiza pato la kigeni kutokana na bei yake ya chini.
Kwa upande mwengine , ujenzi wa reli ya kasi ya SGR na
upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam umesaidia kuimarisha thamani ya mauzo ya
kigeni yanayoingia nchini kwa asilimia 7.8%, ilisema benki ya dunia.
Kulinga na reuters serikali inahitaji kupunguza athari za
kiuchumi kupitia kuimarisha mazingira ya kibiashara na usimamizi wa fedha ,
ilipendekeza benki hiyo.


0 Comments